2017 Februari 5: Jumapili
“Ninyi
ni mwanga wa ulimwengu” (Mathayo 5: 14)
Katika hili, nyota wa zamani wa Uingereza katika runinga za
Malcolm Muggeridge alisema “Siwezi sema ni kwa kiasi gani nimlipe mama Teresa.
Alinionesha ukristo kwa matendo. Alinionesha upendo kwa vitendo. Alinionesha
namna upendo wa mtu mmoja unavyoweza kuanzisha wimbi la upendo ambalo laweza
kuenea dunia nzima”.Mama Teresa alikuwa ni mwanga wa ulimwengu ambaye
aliangazaupendo kuliko kujifanya anapenda.Upendo wake haukuwa wa kujitangaza:
ulikuwa ni moto wa altare.Ulitakiwa ukolezwe na upendo huo uendeleekuwaka;
kwaiyo sala ilikuwa ni muhimu kwake. Mwanga unaotoka kwa Mungu, ni mali ya
Mungu na unatakiwa kuangaza utukufu wake. Kamaupendo uking’aa lakini kwa mtu
pekee unaweza kuwa ni majivuno yaliyojaa
kujionyesha;upendo wa Mungu ni heshima ya kweli. Katika tukio lolote tendo la
utukufu wa Mungu ndiyo furaha kuu ya mwanadamu.
Martin
Luther King Junior alisema, “Giza halifukuzi giza: mwanga tu unaweza kufanya
hilo. Chuki haiwezi kufukuza chuki: upendo unaweza kufanya hilo.” Upendo ni mwanga unaweza kufukuza giza la
chuki. Upole ni mwanga unaweza kufukuza giza la hasira. Kuchapa kazi ni mwanga
unaweza kufukuza giza la uvivu. Kuna mtu mmoja baada ya kuona anapata shida ya
kusali kila wakati wa kulala kwa sababu ya urefu wa sala akaona aiandike sala
yote nakuibandika ukutani, ikifika muda wa kulala anasema: Ee Mungu kama
kawaida hapo ukutani,Amina! Huo ni uvivu. Wakristu walipewa sifa kubwa na Yesu
alipowaita mwanga wa dunia. Lakini sifa hii inawaendea watu wote wanaotenda
mema na kushinda ubaya kwa wema.
Buddha
baada ya kuchunguza mshumaa alisema: “Maelfu ya mishumaa yanaweza kuwashwa na
mshumaa mmoja, na umri wa mshumaa hautafupishwa. Furaha haipungui kwa kuwashirikisha
wengine.” Hupotezi chochote kwa kuwasaidia wengine. “Mshumaa haupotezi chochote
kwa kuwasha mishumaa mingine,” alichunguza hilo katika mishumaa James Keller.
Joyce Meyer alisema hivi: “Biblia inasema kuwa Wakristo ni chumvi ya dunia na
mwanga wa ulimwengu. Kazini, kwenye duka la vinywaji na hata kati ya marafiki
wasio wastaarabu na wanafamilia, Watu wa Mungu wapo kuleta ladha katika hali
mbaya.”
Mwanga
unaonekana na unatusaidia kuona. Mfanyakazi lazima aonekane anafanya kazi.
Kiongozi lazima akuone ili kupandishwa cheo. Mkristo lazima aonekane anakuwa
mkristo jikoni, dukani, kiwandani, hotelini, uwanjani, sokoni, michezoni,
bungeni, barabarani.
“Maneno yote
yatakuwa hayafai kama hayatoki ndani – maneno ambayo hayatoi mwanga wa Kristo
yanaongeza giza” (Mwenye heri Mama Teresa wa Calcutta). Kuwa mwanga wa dunia
kunatudai kutumia maneno ambayo yanatoa mwanga wa Kristo. Tunaweza kusema tusiende mbele ya
wanzetu na midomo mitupu. Midomo ibebe maneno yanayotia mwanga: maneno ya shukrani, maneno
ya kutia moyo, maneno ya kuchangia hoja, maneno ya kusifu, maneno ya msamaha,
maneno ya upendo hayo ni maneno ya kuleta mwanga. Tutafakari methali ya Poland,
“Maneno yapimwe yasihesabiwe.” Yapimwe kama yanafaa au hayafai. Maneno
yanayofaa yanaweza kutusafirisha kutoka kwenye matope hadi kwenye mwezi. Maneno
yenye huruma ni mafupi lakini mwangwi wake unafika mbali. Matusi hayafai badala
yake tumia maneno yenye huruma.
Sala: Ee
Mungu naomba ulimi wangu utoe maneno yanayoleta mwanga, maisha yangu yawe
mwanga wa kuwaangazia wengine, kazi zangu zikupe utukufu, watu waone
wakutukuze. Amina.